Sunday, June 1, 2008

Chatne ya machicha ya nazi




Chatne ni aina ya chachandu yenye asili ya kihindi ,ambayo kazi yake kubwa ni kuongeza hamu ya chakula kama ilivyo kwa aina nyingine za chachandu.

Mara nyingi chatne huliwa na bagia au kachori na pia urojo hasa kwa wale waishio maeneo ya pwani hasa visiwa vya unguja na pemba.

Kuna aina nyingi za chatne kama vile za mapapai ,karoti pamoja na nyinginezo nyingi lakini kama nilivyokueleza mwanzo leo nitakuletea chatne ya nazi.

Mahitaji

Nazi iliyokunwa kikombe 1
Pilipili 3 zilizoiva
Chumvi kijiko kimoja cha chai
Limao au ndimu au hata ukwaju
Pilipili manga za kusaga kijiko kimoja cha chai

Namna ya kutengeneza


Hakikisha nazi unayotumia inakuwa laini na katika hatua ya kwanza unachukua nazi yako
Changanya na pilipili ambayo imesagwa
Weka chumvi halafu
Weka limao ,ndimu au ukwaju .
Changaya pamoja na baada ya hapo weka chumvi pamoja na pilpili manga za kusaga
Baada ya hapo chatne yako itkuwa tayari kwa kuliwa .

No comments:

Post a Comment