Sunday, June 1, 2008

Kababu za mayai



KABABU ni kitafunwa kilichobuniwa kitaalamu zaidi na kukifanya kuonekana cha kuvutia kutokana na umbo na hata ladha yake?

Lakini pamoja na uzuri wake ni watu wachache sana wanafahamu namna ya kutengeneza upishi huu.
Nimeamua kukuletea upishi huu kutokana na maombi ya watu wengi kutaka maelezo ya namna ya kupika kitafunwa hiki.

Fuatana nami upate uhondo huu

mahitaji


Nyama ya kusaga 1/2kg
Mayai 9
kitunguu saumu kiasi
Vitunguu maji kiasi saga
Tangawizi(mbichi) saga
Chumvi kiasi
pilipili manga kiasi
mafuta ya kula lita moja
Mikate wa boflo1
na pilipili kali kiasi kama unatumia.

Namna ya kutengeneza


1) Chukua tangawizi ,kitunguu maji , kitunguu saumu twanga hadi vilainike kisha weka pembeni.
Halafu chukua nyama yako weka chimvi kisha injika jikoni hadi iive halafu ipua.
Chukua mkate wako toa ile nyama ya ndani na kisha uloweke hadi uloanekisha kamua halafu changanya na nyama pamoja na viungo ulivyotwanga kisha weka unga wa pilipili manga huku ukiendelea kuchaganya, ukichanganyika vizuri weka pembeni.
Chukua mayai sita kati ya tisa yachemshe na kisha yamenye halafu weka pembeni.

Chukua mayai matatu yapasue kisha weka chumvi kidogo halafu weka katika bakuli yake.
Tengeneza maduara sita ya kiasi kisha ya huo mchanganyiko kisha weka yai katika kila duara.
Halafu injika jikoni mafuta yakipata moto chovya maduara yako na kisha weka jikoni hadi yawe ya kahawia.Kababu zako

No comments:

Post a Comment