Sunday, June 1, 2008

Katres za nyama ya kusaga



Katres zipo za aina nyingi waweza kupika katres za viazi mbatata, samaki ,nyama na hata mayai .

Lakini leo nitakupa kidogo kuhusiana na katres za nyama .

Mahitaji

Viazi mbatata ¼ kilo
Nyama ya kusaga ¼ kilo
Karoti 1 kubwa
Pilipili hoho 1 kubwa
Chumvi kijiko cha chai
Mayai 5
Mafuta kula lita 1
Kitunguu saumu 1
Kitunguu maji 1
Pilipili mbuzi kiasi unachohitaji .
Unga wa ngano ¼ kilo.
Ndimu 1 kama unatumia

Namna ya kufanya

Chukua viazi mbatata vioshe halafu vichemshe na maganda yake ,baada ya kuiva viweke kwenye maji baridi na kisha menya maganda yake.
Chemsha nyama ikiwa imeunwa na tangawizi au ndimu ili kuondoa shombo na kuifanya iive haraka .
Viweke kwenye kinu na uvisage hadi vilainike kisha weka kwenye bakuli .
Chukua hoho na karoti vikate vidogovidogo halafu weka kwenye bakuli la viazi.
Twanga saumu na kitunguu maji kisha changanya kwenye mchanganyiko wako weka na chumvi na kama itakuwa ndogo ongeza kidogo ili kuleta ladha nzuri na ikiwa unatumia ndimu changanya katika mchanganyiko wako huo .
Weka nyama ya kusaga iliyochemshwa na changanya pamoja .

Baada ya hapo waweza kutengeneza matonge yenye umbo la yai huku ukiyapaka unga wa ngano kuzuia yasigande mikononi fanya hivyo kwa mchaganyiko wote ulio kwenye bakuli.
Chukua mayai yavunje na yamimine kwenye bakuli nyingine iliyo kavu na nyunyuzia ngano kidogo na chumvi .
Weka mafuta kwenye karai na anza kukaanga katres zako chukua tonge moja lichovye kwenye mchanganyiko wa mayai na kulizungushia lote kisha weka kwenye mafuta yanayochemka fanya hivyo kwa matonge yote.

Baada ya hapo katres zako zitakuwa tayari kwa kuliwa waweza kula kwa kinywaji chochote iwe ni cha baridi au hata pombe.

No comments:

Post a Comment