Sunday, June 1, 2008

Sosi ya nyanya



SOSI ya nyanya ni moja kati ya sosi ambazo zinapendwa na watu wengi, kutokana na ladha yake na pia urahisi katika utengenezaji wake.

Kiasili sosi hii imekuwa ikitumiwa sana na wataliano ambapo wao waifahamu kama ‘pomodoro sauce’na mara nyingi wamekuwa wakila na tambi kwa kuwa ndio chakula chao kikubwa.

Lakini je wajua namna ya kutengeneza soso hii? Kwanza kabisa nataka nikujuze kuwa kuwa hii ni sosi ambayo ni rahisi kutengeneza kuliko zile unazozifahamu.

Mahitaji


Nyanya kubwa 2
Kitunguu maji 1
Karoti 1
Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 cha mezani
Mafuta ya kula vijijiko 3 vya mezani
Majani ya vitunguu
Sukari 2½ kijiko
Chumvi kiasi


Namna ya kutengeneza


Chukua mafuta ya kula weka katika sufuria na kisha weka jikoni, baada ya kuchemka anza kwa kukaanga kitunguu saumu, halafu weka kitunguu maji kaanga kwa dakika moja kisha weka slesi za nyanya zikifuatiwa na majani ya kijani ya vitunguu endelea kukoroga, acha vichemke huku ukikoroga kuzuia visiungue kwa muda wa dakika 10.baada ya kuhakikisha kuwa zimeiva weka chumvi na sukari.
sosi yako ipo tayari kwa kuliwa waweza kula na mkate chapati au hata tambi.

No comments:

Post a Comment