Thursday, August 13, 2009

Ni 'blue Iris'


‘Blue iris’ni rangi ya blue iliyokolea na yenye kuwaka, Hii ilikuwa rangi kuu ya dunia kwa mwaka 2008, si hivyo tu kwa mujibu wa wataalamu wa mitindo duniani hii pia imependekezwa kuwa rangi ya msimu kwa sasa ‘colour of season’.

Hivyo basi, kwa kuvaa rangi hii utaonekana ni muelewa wa mitindo na hivyo kuwa wa kisasa zaidi.

Ikiwa una uelewa wa kutosha kuhusiana na suala zima la mitindo nafikiri utakuwa umegundua namna rangi hii ilivyo ‘muhimu’ katika uwanja wa mitindo.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa kipindi hiki kushuhudia warembo wakiwa katika vazi la rangi hii hasa katika mitoko yao ya usiku au shughuli za mchana.

Mavazi ya rangi hii huvaliwa mchana au usiku hii itategemea na namna utakavyolipamba, ikiwa ni maalum kwa usiku yapo mapambo maalum kwa wakati huo vivyo hivyo kwa mchana.

‘Blue iris’inaendana na rangi gani?

Zipo rangi ambazo zikivaliwa na rangi hii huonekana kuvutia zaidi kuliko pale zinapovaliwa peke yake ambapo kwa mujibu wa wataalamu rangi nyeusi na njano na fedha ndio hasa rangi sahihi zinazoendana na rangi hii.

Unaweza kuvaa nguo yanye rangi ya blue na kujipamba kwa kutumia mapambo ya njano, vilevile unaweza kuvaa nguo ya njano na kuinakshi kwa kutumia mapambo blue iris hii ni kwa wakati wa mchana.

Pia si vibaya ikiwa utalipamba vazi hili kwa kutumia rangi ya pink, kwani utaonekana upo juu pia katika mitindo.

Ikiwa utaamua kuvaa vazi la rangi hii kwa wakati wa usiku, italeta maana zaidi ikiwa utaipamba vazi lako kwa rangi ya fedha, kwa kuvaa mapambo yenye rangi hiyo.

Kwa mfano unaweza kuvaa viatu, hereni bangili au kubeba pochi iliyonakshiwa kwa rangi ya fedha hapo utaonekana upo juu zaidi katika mitindo kuliko vile unavyofikiria.

Umuhimu wa rangi ya blue iris katika mitindo.
‘Blue Iris’ ni rangi yenye sifa ya kike, pia inaaminika kuwa endapo itatumika kwa mapambo ndani ya nyumba ina uwezo mkubwa wa kufukuza majini au mapepo katika nyumba na kuiacha huru.

Pamoja na kuvutia kwake rangi hii ina sifa ya kumfanya mvaaji aonekane mwembamba zaidi ya umbo lake halisi. Pia ni rangi ya kujiamini kutokana na uwezo wake wa kuweza kuonekana kwa haraka.

Rangi hii ina sifa zinizofanana na rangi ya njano, hot pink na rangi nyingine zinazofanana hizo, kitendo cha kuonekana haraka kabla ya nyingine hujenga hisia ya kujiamini kwa mvaaji husika.

No comments:

Post a Comment