Saturday, September 12, 2009

Gladiator sandals zipo 'in' nazo





Aina hii ya viatu vimekuwa vikipendelewa na watu mbalimbali wakiwamo, mastaa uzuri wake ni kwamba unaweza kuvaa na nguo aina yeyeto na kutoka bomba.

Saturday, September 5, 2009

Ujumbe wa leo

Mtume Mohammad(s.a.w) alisema itakuja zama ambazo watu watapenda mambo 5 na kusahau mambo 5.

1.Watapenda DUNIA na watasahau AKHERA.
2.Watapenda MALI zao na watasahau HESABU za matendo yao .
3.Watapenda VIUMBE wenzao na watasahau MUNGU wao.
4.Watapenda MAOVU na kusahau TOBA.
5.Watapenda MAJUMBA yao na kusahau MAKABURI yao .

TUMUOMBE MWENYEEZI MUNGU ( s.w. ) ATUEPUSHE NA SAHAU HIZO.

Ramadhani Karim!!!!!

Friday, September 4, 2009

Kitafunwa cha leo


Mabawa ya kuku/chicken wings

Tukiwa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, si vibaya tukaelekezana vyakula vidovidogo vinavyoweza kuliwa mara baada ya futari hususani kwa ajili ya kuchangamsha mdomo.
Leo nimekuandalia mabawa ya kuku au vipapatio kama wengi wanavyopenda kuviita

Mahitaji

Mabawa ya kuku 1/2 kg pilipili manga1/2 kijiko cha mezani chumvi 1 cha mezani
Kitunguu saumu cha kusaga kijiko kimoja 1 sosi ya soya kijiko 1 cha mezani.juisi ya limao vijiko 2 unga wa ngano vijiko 2 vya mezani.
Sosi kali ya ‘periperi’chumvi kijiko 1 cha mezanikitunguu saumu kijiko 1 cha mezanimafuta ya kula ½ kikombe.½ vinegajuisi ya limao vijiko viwili unga wa pilipili nyekundu vijiko viwili.pilipili nzima za kuiva 4-5 pilipili za kashmiri 6
Namna ya kutengeneza

Weka pilipili za Kashmiri, pilipili nzima za kuiva na unga wa pilipili kwenye kikombe cha maji kwa usiku mmoja.
Baada ya hapo saga kwenye blenda kwa muda wa dakika tano.
Weka kwenye bakuli lenye mfuniko na kisha hifadhi kwenye jokofu.

Chukua mabawa ya kuku na yaoshe vizuri kisha yaweke kwenye chombo au bakuli lenye nafasi,
Weka viungo vyote halafu viache kwa muda wa masaa mawili hadi matatu.
Baada ya hapo weka karai la mafuta jikoni tayari subiri hadi yapate moto
Weka jikoni na kaanga hadi viwe na rangi ya hudurungi.

Chakula chako tayari kwa kuliwa andaa chakula hicho pamoja na sosi yako ya periperi ili uweze kupata ladha halisi.

MJ kuzikwa leo


Hatimaye Mfalme wa Pop,Michael Jackson,anatarajiwa kuzikwa leo huko Forest Lawn-Glendale,California katika makaburi yajulikanayo kama Holly Terrace.Mazishi yanatarajiwa kuanza saa moja usiku kwa saa za California.
Kwa mujibu wa taarifa kuhusu mazishi hayo,yatakuwa ni mazishi “private” na hivyo ni ndugu,jamaa na marafiki wa karibu pekee watakaoweza kuhudhuria.

Mazishi hayo yanafanyika baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kina wa kifo chake.

Hivi karibuni Mchunguzi wa vifo wa California,alithibitisha kwamba Michael Jackson alifariki dunia kutokana na kuchomwa sindano ya kupunguza maumivu ambayo ilikuwa na dozi kubwa kuliko kawaida. Daktari aliyekuwa naye siku hiyo,Dr.Murray, ndiye anatupiwa lawama zote ingawa mpaka leo hakuna mashtaka rasmi kuhusiana na kifo cha mwanamuziki huyo.


KALALE PEMA PEPONI MICHAEL JOSEPH JACKSON